Meulensteen, ambae alikuwa Kocha chini ya himaya ya Sir Alex Ferguson kwa Miaka 12, amesema hivi sasa Man United imepanda kidogo baada ya mwanzo mgumu na hiyo ni kwa sababu ya kazi nzuri ya Meneja Louis van Gaal.
Hata hivyo, Meulensteen amekiri kuwa Man United bado ina udhaifu kwenye Difensi na anategemea Jose Mourinho kujua hilo na kutumia udhaifu huo kama mwanya.
Akiongea na Sky Sport, Meulensteen alisema: “Ikiwa tunazungumzia uwezo wa Mpinzani, ni kweli Man United wana mtihani mgumu kwani Chelsea wanaongoza Ligi na wako Pointi 10 mbele ya Man United. Lakini itakuwa ni msukumo mkubwa kwa United kama wataweza kushinda. Ushindi huzaa imani na hilo ndio United wanataka. Wanahitaji mbio ndefu za ushindi na wakianza na Chelsea hiyo ni hatua kubwa.”
Meulensteen aliongeza: “Ni wazi Van Gaal amebadili mfumo mara kadhaa. Alijaribu ule mfumo wake maarufu 3-5-2 mapema mwanzoni mwa Msimu lakini sasa amerudi Difensi ya Watu Wanne na hilo linawafaa United. Lakini wamesuasua hasa kutokana na kuwa na Majeruhi wengi na hajapata Difensi iliyotulia na hilo huzifanya Timu zijue zitapata Magoli.”
Kuhusu Chelsea, Meulensteen alisema: “Mourinho atakuwa ameshafanya utafiti wa kutumia udhaifu wa United. Hujui atafanya nini pengine Didier Drogba atacheza badala ya Diego Costa. Anaweza hata kumweka Eden Hazard mbele kwa sababu ya kasi na nguvu. ”
Kila Timu itawakosa Mastaa wao kadhaa na Man United haitakuwa na Nahodha wao Wayne Rooney ambae ndie anamalizia Kifungo chake cha Mechi 3 kwenye Mechi hii baada ya kulambwa Kadi Nyekundu huku Chelsea wakiwakosa Mastraika wao Majeruhi Diego Costa na Loic Remy.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
MAN UNITED: David De Gea, Rafael, Jones, Smalling, Rojo, Carrick, Blind, Fellaini, De Maria, Falcao, Van Persie
CHELSEA: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Luis, Matic, Fabregas, Willian, Oscar, Hazard, Schurle
REFA: Phil Dowd
0 comments:
Post a Comment