
TAMASHA
la Siku ya Msanii lililofanyika jijini Dar es Salaam jana usiku,
litaendelea kubakia kwenye historia ya aina yake baada ya kubeba hadhii
ya kipekee – lilikuwa ni tamasha bab kubwa, mandhar bab kubwa, show bab
kubwa, mgeni rasmi bab kubwa, tuzo bab kubwa.
Mgeni rasmi katika tamsha hilo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohammed Gharib Bilal.
Aina
ya watu waliojazana ukumbuni, aina ya mavazi yalitotawala ukumbini,
aina ya burudani zilizotolewa na nidhamu iliyokuwepo, inafanya tamasha
hilo lililofanyika Mlimani City, liwe sahihi kwa watu wa rika zote –
wakubwa na wadogo.
Zikatolewa tuzo mbili mahsusi: Tuzo ya
msanii aliyejitolea maisha yake yote katika sanaa ambayo ilikwenda kwa
mchoroji maarufu Edward Said Tingatinga mwenye maskani yake Masasi
mkoani Mtwara. Tuzo ya pili ni ya msanii aliyetumia sanaa kuitumikia
jamii kwa maisha yake yote ambayo ilikwenda kwa Father Kanuti, mmoja wa
watu waliowafundisha wanamuziki wengi sana hapa nchini.
Siku ya msanii Siku
Ya Msanii iliandaliwa na Haak Neel Production kwa kushirikiana na
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na New Habari |(2006)
LTD kupitia magazeti ya Dimba, Bingwa, Mtanzania na The African, Azam
Media, Ledger Plaza Hotel, CXC, Proin Tanzania, Channel Ten, Magic FM,
Clouds FM, EFM.
Washindi wa tuzo walipewa bakshishi ya shilingi milioni moja kila moja, lakini kama vile hiyo haitoshi, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal
akawaongeza milioni tano kila moja na kufanya kila mshindi aende
nyumbani na kitita cha shilingi milioni 6.
Burudani
zilizorindima ukumbini mbali na sarakasi na ngoma za asili na show za
madansa, pia kulikuwa na uhondo kutoka kundi la The Kilamanjaro Band
“Wana Njenje”, Isha Mashauzi, Diamond, Yamoto Band na wavunja mbavu
kutoka Kenya Erick Omondi na Fred Omondi.
Lakini
tamasha hili ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka Oktoba 25,
lilipambwa pia na maonyesho ya mavazi yaliyoandaliwa na Fabak Fashion
chini yake Asiya Idarus.
Pata picha kadhaa za tamasha hilo la aina yake.
Safu ya viongozi wa serikali ikifuatilia tamasha la Siku ya Msanii
Madansa wa Extra Bongo chini ya Super Nyamwela
Hiyo ni tuzo aliyopewa Father Kanuti
Isha Mashauzi akipiga bonge la show
Mashauzi na madansa wake wakiendelea na makamuzi
Ni wakati wa fashion show
Ako Mpiluka Band wakali wa kupiga nyimbo za asili kwa kutumia ala za kisasa
Mwanaume kazini!
Uhondo wa ngoma za utamaduni
MC wa tamasha la Siku ya Msanii Jokate (kushoto) akinyongesha kiuno na Nyota Waziri
Nyota Waziri akifanya yake
Ni wakati wa Diamond kufanya yake
Diamond akiendelea kupagawisha
Kazi bado inaendelea kwa Diamond na mashabiki wake
Si mchezo
Si uchawi ni mazoezi
Tingatinga akipokea tuzo yake kutoka kwa Makamu wa Rais
Wachekeshaji kutoka Kenya
Achana kabisa na hawa watu
Yamoto Band wakishambulia jukwaa
Yamoto Band
Si chura huyu, ni binadamu
Jamaa alijua kucheza na mwili wake
Fashion haina umri wala umbo! hapo ni mwanamuziki Abdul Salvador,Asia Idaurus
0 comments:
Post a Comment