Staa wa kimataifa wa Wales anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Gareth Bale ameingia
katika TOP 3 ya wachezaji wa soka wanaolipwa pesa ndefu zaidi duniani
ambapo ameingia katika list hiyo kutokana na mkataba wake mpya na Real Madrid.
Kwa sasa Bale atakuwa akilipwa pound 346,000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 900 ambapo katika kipindi cha miaka sita Bale atakuwa kaingiza jumla ya pound milioni 108.
Bale sasa anakuwa katika TOP 3 hiyo wakati kwa wachezaji wa Afrika, kiungo wa Man City na raia wa Ivory Coast Yaya Toure yupo
nafasi ya 10 katika list ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa
duniani licha ya kuwa yupo katika wakati mgumu wa kujua hatma yake chini
ya Guardiola.
0 comments:
Post a Comment