Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Jay Moe amesema
ukimya wake kwenye game la muziki umemfanya ajue wasanii wenzake huwaga
wanakosea wapi.
Rappa huyo ambaye amedai amekaa miaka 4 bila kutoa ngoma yake binafsi, ameiambia Bongo5 kuwa amegundua style mpya ambavyo itamfanya afanye vizuri zaidi.
“Unajua kuna kitu fulani kama malaika anakwambia acha hiki fanya hiki, alafu kweli unakifanya na unaona kabisa leo kinaleta manufaa, nimejifunza vitu vingi sana, sasa hivi wasanii wenzangu wanakuja na nyimbo mpya sometime nakuta nacheka, naona mbona nyimbo hii bado haipo kwenye muziki wa siku hizi. Hii time ambayo nilikuwa nje ya muziki nimejikuta nimesoma vitu mpaka vilivyo mbele yangu,” alisema Jay Moe
Aliongeza, “Pia ukimya wangu nilikuwa napanga mambo mengine nje ya muziki, hatuwezi tukafocus kwenye muziki tu, tumeshakuwa watu wazima wengine, huko tunakoelekea tutafanya muziki labda miaka 4 tu. Hatuna muziki wa Marekani wa kuona akina Dr Dre bado wananufaika kazi zao mpaka leo,” alisema Jay Moe.
Jay Moe ameachia ngoma yake mpya ‘Pesa ya Madafu’ iliyotayarishwa na Daz Naledge kupitia studio za Bongo Records.
SIKILIZA NA PAKUA WIMBO HUU HAPA

0 comments:
Post a Comment