BAADA
ya kile kichaa cha kuwa na Blackberry kwisha, nikaamua kuiuza nikanunua
kitu kutoka China, bonge la simu, chuma mtupu zito hilo nikikupiga nalo
kichwani hauamki ila lina kasheshe hilo ukichaji dakika tatu tu
linaonyesha full Charge, ila lina TV, touchscreen, kijiko , uma,
nailcutter choo na bafu. Mara nyingine ukianza kuandika meseji simu
inajiandikia mambo yake inayotaka yenyewe, mpaka uzime halafu uanze
tena. Ukipita karibu na Mchina inaandika ‘One Bluetooth device found’
Akipita demu mzuri inaandika WIFI found, akipita mbaya inaandika Virus
detected. Nataka kuiuza lakini vituko vyake vinanifanya nione tabu
kuiuza.
CHECK me!!!!
Sunday, January 11, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment