Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, January 23, 2015

AFCON_BAO LA DAKIKA ZA LALA SALAMA LA GYAN LAIZAMISHA ALGERIA USIKU HUU.


Asamoah Gyan ambaye amerudi kutoka majeruhi ameibua matumaini ya Ghana katika harakati ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Afcon 2015 inayoendelea huko nchini Equatorial Guinea.
Ghana ambayo ilipoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa bao 2-1 ilimkosa mshambuliaji wake huyo kutoka na na kusumbuliwa na Malaria.
Matokeo hayo yamelifanya kundi C kuwa gumu zaidi kutokana na timu zote kuwa na alama tatu isipokuwa Afrika ya kusini ambayo ilipoteza mchezo wake wa awali dhidi ya Algeria.
Mchezo mwingine wa kundi hilo utaendelea majira ya saa 4 usiku huu kwa majira ya Afrika ya Mashariki wakati Senegal watapambana na Afrika ya kusini.
Vikosi vilivyoanza kwa timuzote mbili vilikuwa ni hivi. 
Ghana XI: Brimah, Afful, Rahman, Amartey, Mensah, Acquah, A. Ayew, Badu, Atsu, Gyan, J. Ayew
Algeria XI: M'Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Lacen, Taider, Bentaleb, Brahimi, Feghouli, Belfodil

Related Posts:

0 comments: