Wanaume
wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi
kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake
wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata
wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali
sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na
sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti
ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna
kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili
aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi
kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu
kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo
kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa
mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio
wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi
kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama
kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya
dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua
tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume.
Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu
lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza
kufifia.
Kwanini
wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao
na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba
maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda
na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama
itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima
afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote
wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si
hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi,
kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia
ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi
yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha
mustarehe.
WENYE TABIA NZURI
Tabia
njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda,
hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia
inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa
sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile
mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa
anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa
baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja
kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau
suala hilo la tabia.
Si
hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa
kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache
yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa
ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi
karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa
hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'.
Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma
kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio
vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata
vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na
kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na
wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye
ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi
lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye
ili wafanikiwe.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna
wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza
kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali
hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila
wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake
kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba
uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi
sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi
cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza
hata kupunguza mapenzi.
Wanawake
kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa
kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume
atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila
atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune
mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au
leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi
nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu
fulani.’
Wanaume
ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote
ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho
kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa
bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna
wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea
hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au
wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi
kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu
kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona
kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa
utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi
wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati
inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo
wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba
maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama
kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke
anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea
anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa
kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa,
kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama
nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu
kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama
nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima
atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote,
yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi
wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha
ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu,
wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo
kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio
wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia,
wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti
huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake
ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana
hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume
wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa,
kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza
yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu.
Waweza kubadilika kwani inawezekana.
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingi utamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya. Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini. Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?" Akimuona rafiki yake kanunua simu ya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia, "mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitaji upo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana uwezekano haupo.
WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali jijini Dar-es-Salaam. Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
0 comments:
Post a Comment