Kipindi cha kwanza cha mchezo unaoendelea wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya watani wawili wa jadi Yanga Vs. Simba mabao bado ni bila bila (0 _0) na katika mchezo huu unaoendelea katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam timu zote mbili zimeonekana zikiwa na kasi ya hali ya juu licha ya tegemezi wa yanga ambaye ni Continho ameonekana kupeleka mashambulizi kwenye lango la Simba,hata hivyo katika kipindi hiki cha kwanza yanga wamepata kona tatu na simba hawajapata hata moja,
Pia katika michezo mingine inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Coastal union 1_Vs.Mgambo jkt _0 goli ambalo limefugwa na Ramadhani kwa mkwaju wa penati, mchezo ambao unaendelea katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,pamoja na mchezo mwingine kati ya Ruvu shooting _1 Vs.Ndanda Fc ya Mtwara ambapo hawa ndanda ni wenyeji wa mchezo huu.
0 comments:
Post a Comment