Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, October 31, 2016

Dalili 10 ukiziona tu, tambua unakaribia kufukuzwa kazi

 Wataalamu wa mambo ya Saikolojia wametuletea hii kuhusu dalili ambazo ukiwa mfanyakazi au muajiriwa kwenye kampuni yoyote halafu ghafla ukaanza kuona kuna mabadiliko kwa maboss wako tofauti walivyokuwa mwanzo basi jua kuna jambo gumu linafata kwako.
Hakuna mtu anaweza kufurahia taarifa ya kufukuzwa kazi  japokuwa ni ngumu pia kuwa na uhakika wa ulinzi wa ajira yako. Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Saikolojia baada ya kuzungumza na watu waliofukuzwa kazi wengi wao walikiri kushtushwa na taarifa hizo ingawa wameeleza kuwa kuna dalili walianza kuziona wakiwa ofisini lakini hawakudhani kama ilikuwa njia ya kuelekea kutimuliwa.
Na ili kukuokoa kabla mambo hayajaharibika ni vema ukaanza kuandaa CV zako mapema. Nimekuwekea hapa dalili 10 za kugundua kama umechokwa ofisini kwako au na mwajiri wako na wanapanga kukuwashia moto.
  1. Majukumu Yasiyoeleweka: Mwanzo wakati unaanza kazi mambo yalikua safi lakini ghafla boss wako anaanza kukupangia majukumu mengine na ni yale ambayo anajua kabisa huna uwezo nayo au anakupa majukumu yasiyo na faida yoyote kwake na kwako!
  2. Haupewi nafasi ya kukutana na Boss wako. Muajiri wako anaanza kukukwepa au hakupi nafasi ya kuongea naye kama mwanzo, na hakupi majukumu yenye faida.
  3. Boss hapendi kukutana na wewe: Ni jambo la kushangaza inakuaje mtu aliyekua anakuamini sana ghafla inatokea hapendi kukutana na wewe iwe ni kwa issue za kiofisi au binafsi wakati mwanzo alikua anakushirikisha hadi mambo yake binafsi.
  4. Mipango au ushauri: Mwanzo ulikua mtu wa kwanza kuombwa ushauri na ulikua unaonekana ni wa maana sana unaanza kuonekana hauna nguvu wala ushawishi tena. Hauoni ushauri wako ukifanyiwa kazi kama mwanzo.
  5. Boss wako anatafua makosa: Vitu vidogo sana ulivyofanya vinakuzwa na unafokewa sana wakati mwingine unakua hata haujahusika.
  6. Unatakiwa kuwafundisha wengine: Sio jambo baya lakini ni la hatari inapotokea boss wako anaanza kukwambia uanze kuwafundisha watu wengine majukumu yako hasa waliokuwa chini yako. 
  7. Unajadiliwa sana kwenye vikao: Muda mwingi Boss wako anazungumza na HR kuhusu utendaji wa wafanyakazi na milango inakua imefungwa, ukiingia tu wananyamaza mpaka utoke.
  8. Haualikwi kwenye Vikao muhimu: Zamani ulikuwa wa kwanza kuambiwa chochote kuhusu vikao vya ofisi pamoja na maamuzi au mabadiliko yoyote ila sasa haushirikishwi kwa lolote.
  9. Unaombwa kuandika majukumu yako mara kwa mara: Ni jambo la ajabu sana, Boss wako ndiye aliyekupangia majukumu yako wakati unaajiriwa lakini ghafla anaana kukwambia umuandikie kazi unazofanya kila siku. Hapo anza kupanga vitu vyako. 
  10. Unatakiwa kueleza umefanya nini kwenye kampuni: Boss wako anakutaka umuandikie umefanya nini kwenye ofisi yake tangu ulipoajiriwa na unategemea kufanya nini kipya.

0 comments: