Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Sunday, October 26, 2014

RAY C, AFUNGUKA,HAYA_ WAKATI CHID BENZ AKISOTA POLISI


ray c
“Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua
sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema………Tanzania Stand Up with Him.

Related Posts:

0 comments: