Nyota wa muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim.
Musa Mateja
WENYE wivu wajinyonge! Nyota wa
muziki wa kizazi kipya, zao la BSS 2012 Meninah Abdulkarim, anadaiwa
kufunga ndoa kimyakimya mwishoni mwa wiki iliyopita na mtu anayetajwa
kulelewa tangu utotoni na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
aliyejiuzulu, Profesa Sospeter Muhongo, Risasi Mchanganyiko limetonywa.
Chanzo chetu makini kimearifu kuwa
shughuli hiyo ilifanyika Agosti 16 mwaka huu ikimaliziwa na sherehe
kubwa iliyofanywa nyumbani kwao, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Ebwana
Meninah kaolewa na jamaa mmoja ambaye tumeambiwa ni mtoto wa Muhongo,
ambaye alikuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu sasa,
ndoa hiyo ilikuwa ya siri maana sisi hatukujua kabisa, ila nilikuwa
naenda zangu mjini mara nikakutana na magari ya harusi ndiyo nikajumuika
na mimi kula ubwabwa,” kilisema chanzo chetu ambacho kilishuhudia
shughuli nzima.
Inadaiwa kuwa bwana harusi amelelewa kwa
muda mwingi wa maisha yake na Profesa Muhongo kiasi kwamba watu wa
karibu na familia hiyo walifahamu ni mtoto wake wa kumzaa. Hata hivyo,
haikuweza kujulikana mara moja uhusiano baina ya Profesa na bwana harusi
huyo, anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara mzuri hapa nchini.
Gazeti hili liliwasiliana na kaka yake
Meninah ambaye pia ni meneja wake, Atik Abdulkarim ambaye alikiri dada
yake kufunga ndoa, lakini akashangaza baada ya kudai hafahamu jina la
shemeji yake, ingawa alisema ni kweli mume ni mtu aliyelelewa na Profesa
Muhongo.
“Ni kweli Meninah kaolewa jana
(Jumapili), ila jina la bwana harusi mimi silijui maana nimezoea kumuita
shemeji tu,” alisema Atik.
0 comments:
Post a Comment