Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili, Rose Muhando.
Brighton Masalu
MWIMBAJI nyota wa nyimbo za
Injili, Rose Muhando, amewaomba radhi watu wote aliowahi kuwakwaza,
ikiwa ni pamoja na kuchukua fedha za kushiriki onesho, lakini akashindwa
kufanya hivyo, akidai ni ubinadamu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Rose
alikiri kuingia baadhi ya mikataba na kushindwa kuitekeleza, akisema ni
jambo lililomkosesha sana raha, hasa pale watu walipokuwa wakimchukulia
kama tapeli.
“Hata hivyo, mara nyingi huwa
nasingiziwa, lakini nakaa kimya kwa sababu nimeumbwa hivyo, kama kuna
yeyote nimemdhulumu naomba anisamehe, sikufanya makusudi, nilishindwa
kutokea kwa bahati mbaya, mimi ni binadamu. Namuomba pia baba yangu
mlezi Msama (Alex, Meneja wake) naye kama kuna mahali nilimkwaza kwa
matamshi au matendo, naomba anisamehe,” alisema nyota huyo wa kibao cha
Facebook.
0 comments:
Post a Comment