Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Sunday, October 26, 2014

VAN PERSIE ASAWAZISHA DAKIKA YA MWISHO, UNITED 1 CHELSEA 1!

LIGI KUU ENGLAND

MATOKEO:
Jumapili Oktoba 26
Burnley 1 Everton 3
Tottenham 1 Newcastle 2
Man United 1 Chelsea 1
+++++++++++++++++++++++
MANUNITEDvCHELSEAKwenye Mechi iliyochezwa Old Trafford, Robin van Persie aliifungia Manchester United Bao katika Dakika ya mwisho ya Dakika 4 za Majeruhi na kuipa Sare ya Bao 1-1 na Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea.RVP-ASAWAZISHA
Chelsea walitangulia kupata Bao kupitia Didier Drogba ambae alifunga kwenye Dakika ya 53 kwa Kichwa baada ya Kona ya Cesc Fabregas.
Ingawa Man United walimiliki zaidi Mpira na kulenga Mashuti mengi zaidi ya Chelsea lakini ule udhaifu wao wa Difensi, hasa kulinda Mipira ‘iliyokufa’ kumewagharimu kwa mara nyingine tena.
Huku Bango likiashiria zipo Dakika 4 za Nyongeza baada ya Dakika 90 kukamilika, Chelsea walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 93 baada ya Branislav Ivanovic kulambwa Kadi ya Njano ya MANUNITEDv CHELSEA-TAKWIMUPili kwa kumsukuma Angel Di Maria na kupewa Kadi Nyekundu.
Frikiki iliyofuatia ilipigwa na Angel Di Maria na kukikuta Kichwa cha Marouane Fellaini lakini Kipa Thibaut Courtois akaokoa na kumtemea Robin van Persie ambae alipachika Mpira wavuni na kuamsha shangwe kubwa Ndani ya Old Trafford.
Hata hivyo, Sare hii imewapaisha Chelsea kileleni wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Southampton na Pointi 6 mbele ya Timu ya 3 Mabingwa Man City.
Man United wao wamebakia Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Chelsea.
Mechi inayofuata kwa Manchester United ni ule mtanange wa Dabi ya Manchester watakapotua Etihad kupambana na Mahasimu wao wakubwa Manchester City Jumapili Novemba 2.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea; Rafael, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Fellaini; Di Maria, Mata (Wilson - 67'), Januzaj, Robin van Persie
Akiba: Lindegaard, Blackett, Fletcher, Carrick, Herrera, Pereira, Wilson.
CHELSEA: Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry, Felipe Luis, Matic, Fabregas, Willian (Zouma - 93'), Oscar (Mikel - 67'), Hazard (Schürrle - 90'), Drogba
Akiba: Cech, Zouma, Ake, Mikel, Schurrle, Baker, Salah.
REFA: Phil Dowd
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Oktoba 27
2300 QPR v Aston Villa

MSIMAMO
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
9
15
23
2
Southampton
9
15
19
3
Man City
9
9
17
4
West Ham
9
5
16
5
Arsenal
9
4
14
6
Swansea
9
3
14
7
Liverpool
9
1
14
8
Man United
9
3
13
9
Everton
9
2
12
10
Hull
9
0
11
11
Tottenham
9
-2
11
12
Stoke
9
-2
11
13
West Brom
9
-1
10
14
Newcastle
9
-5
10
15
Aston Villa
8
-8
10
16
Crystal Palace
9
-3
9
17
Leicester
9
-4
9
18
Sunderland
9
-9
8
19
Burnley
9
-11
4
20
QPR
8
-12
4

LIGI KUU ENGLAND
_RATIBA-Mechi zijazo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 1
1545 Newcastle v Liverpool
1800 Arsenal v Burnley
1800 Chelsea v QPR
1800 Everton v Swansea
1800 Hull v Southampton
1800 Leicester v West Brom
1800 Stoke v West Ham

Jumapili Novemba 2
1630 Man City v Man United
1900 Aston Villa v Tottenham

Jumatatu Novemba 3
2300 Crystal Palace v Sunderland

Related Posts:

0 comments: