LICHA ya kuwa kocha wa Liverpool Brendan
Rodgers amekuwa akimkingia kifua mshambuliaji wake Mario Balotelli,
lakini ni wazi kuwa kocha huyo sasa anaanza kuangalia mipango mingine ya
kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Baada
ya Balotelli kukosa bao la wazi akiwa hatua tatu tu kutoka langoni
katika mchezo wa Ligi Kuu wa sare ya 0-0 dhidi ya Hull City, ikiwa ni
mechi ya pili mfululizo kupoteza nafasi ya wazi, Brendan Rodgers sasa
anataka kumsajili Saido Berahino wa West Bromwich Albion.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa ‘Under 21’ ya England, amekuwa pia akiwaniwa na
Tottenham Hotspur ambapo ofa ya pauni milioni 15 imekuwa ikihusishwa na
klabu hiyo kutoka kaskazini mwa London.
Hata
hivyo West Bromwich inaamini Berahino ana thamani ya pauni milioni 25
na ujio wa Liverpool kwenye mpango huo, utapelekea vita vya kuonyeshana
nguvu ya pesa kati yao na Spurs.
Liverpool
imebaini wazi kuwa kumsajili Balotelli ilikuwa ni kamari ambayo
haijalipa na itaangalia uwezekano wa kummuvuzisha kwenye dirisha dogo la
Januari.
Habari za ndani zinasema hata kama Liverpool watashindwa kumhamisha, lakini bado watasajili mshambuliaji mwingine.
0 comments:
Post a Comment