Jumanne Usiku zipo Mechi 5 ambazo ni pamoja za Vigogo Chelsea kucheza Ugenini na Shrewsbury, Timu ya Daraja la Ligi 2 ambalo ni Madara matatu chini ya Ligi Kuu, wakati Liverpool watakuwa kwao Anfield kucheza na Swansea City, pambano linalohusisha Timu za Ligi Kuu England pekee.
Jumatano yapo mapambano mawili ya Timu za Ligi Kuu England pekee ambayo ni huko Etihad kati ya Mabingwa wa England na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Man City, dhidi ya Newcastle, na jingine ni lile la Stoke City v Southampton.
Siku hiyo hiyo, Tottenham watakuwa kwao White Hart Lane kucheza na Brighton City ambayo inacheza Daraja la Championship ambalo ni chini tu ya Ligi Kuu England.
Washindi wa Raundi hii ya Nne watatinga Robo Fainali ambayo Droo yake itafanyika kesho kutwa na Mechi zake kuchezwa Wiki ya Desemba 14.
CAPITAL ONE CUP
RAUNDI YA 4
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumanne Oktoba 28
2245 Bournemouth v West Brom
2245 MK Dons v Sheffield United
2245 Shrewsbury v Chelsea
2300 Fulham v Derby
2300 Liverpool v Swansea
Jumatano Oktoba 29
2245 Man City v Newcastle
2245 Stoke v Southampton
2245 Tottenham v Brighton
++++++++++++++++++++++++++++++
MFUMO
-RAUNDI YA 5 [Robo Fainali]
–Wiki ya Desemba 14
-Droo kufanyika – Oktoba 29
NUSU FAINALI
-Droo – Desemba 17
-Mechi za Kwanza – Wiki ya 19 Januari 2015
-Mechi za Marudiano - Wiki ya 26 Januari 2015
FAINALI
–Jumapili 1 Machi 2015
0 comments:
Post a Comment