Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, October 27, 2014

FIFA BALLON d’Or: JUMANNE RONALDO KUJUA WAPINZANI WAKE, MAJINA 23 KUTOLEWA!


RONALDO-Fifa Ballon dOr2013JUMANNE OKTOBA 28, FIFA inatarajiwa kutangaza Listi ya awali ya Wagombea 23 wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d’Or,  kwa Mwaka 2014 na miongoni mwao atakuwepo Cristiano Ronaldo ambae alitwaa Tuzo hii Mwaka Jana.

Mwaka 2013, Ronaldo anaechezea Real Madrid, alitwaa Ballon d’Or na kuvunja wimbi la Lionel Messi la kutwaa Tuzo hiyo kwa Miaka Minne mfululizo.

Majina hayo ya Wagombea 23 yatateuliwa na Kamati ya Soka ya FIFA ikishirikiana na Wataalam kutoka Jarida la France Football ambao ndio Waasisi hasa wa Ballon d’Or.

Kuanzia Mwaka 2010, France Football waliungana na FIFA na kuziunganisha Tuzo za Ballon d’Or pamoja na ile ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na kuitwa FIFA Ballon d’Or.

Listi hii ya Wagombea 23 inatarajiwa kupunguzwa hadi Wachezaji Watatu ifikapo Desemba na hao ndio watakaoingia Fainali ambayo Mshindi wake atatokana na Kura za Wanahabari wa Soka maalum, Makocha wa Timu za Taifa Duniani na Makepteni wa Timu hizo.
Mshindi wa FIFA Ballon d’Or kwa Mwaka 2014 atatangazwa hapo Januari 12, 2015 huko Zurich, Uswisi kwenye Kongresi ya FIFA, iitwayo Zurich Kongresshaus.

Kwenye kugombea Tuzo ya sasa, Ronaldo anatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa Messi na Neymar, wote wa Barcelona, na pia Wachezaji kutoka Mabingwa wa Dunia Germany, Kipa Manuel Neuer na Nahodha wao Philipp Lahm, na mwenzao wa Bayern Munich, Arjen Robben

WASHINDI WALIOPITA WA Ballon d'Or:
1956 Stanley Matthews
1957 Alfredo Di Stefano
1958 Raymond Kopa
1959 Alfredo Di Stefano
1960 Luis Suarez
1961 Omar Sivori
1962 Josef Masopust
1963 Lev Yashin
1964 Denis Law
1965 Eusebio
1966 Bobby Charlton
1967 Florian Albert
1968 George Best
1969 Gianni Rivera
1970 Gerd Muller
1971 Johan Cruyff
1972 Franz Beckenbauer
1973 Johan Cruyff
1974 Johan Cruyff
1975 Oleg Blokhin
1976 Franz Beckenbauer
1977 Allan Simonsen
1978 Kevin Keegan
1979 Kevin Keegan
1980 Karl-Heinz Rummenigge
1981 Karl-Heinz Rummenigge
1982 Paolo Rossi
1983 Michel Platini
1984 Michel Platini
1985 Michel Platini
1986 Igor Belanov
1987 Ruud Gullit
1988 Marco van Basten
1989 Marco van Basten
1990 Lothar Matthaus
1991 Jean-Pierre Papin
1992 Marco van Basten
1993 Roberto Baggio
1994 Hristo Stoichkov
1995 George Weah
1996 Matthias Sammer
1997 Ronaldo
1998 Zinedine Zidane
1999 Rivldo
2000 Luis Figo
2001 Michael Owen
2002 Ronaldo
2003 Pavel Nedved
2004 Andriy Shevchenko
2005 Ronaldinho
2006 Fabio Cannavaro
2007 Kaka
2008 Cristiano Ronaldo
2009 Lionel Messi
2010 Lionel Messi
2011 Lionel Messi
2012 Lionel Messi
2013 Cristiano Ronaldo

Related Posts:

0 comments: