Kibosile Ivan Ssemwanga akiwa na ‘Zari’.
Umaarufu wa msanii wa muziki, mjasiriamali na mkali wa fasheni kutoka
Uganda anayeishi Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari’ unazidi kupaa
kila kukicha, habari ya mjini kwa sasa ikiwa ni malavidavi ya nguvu
anayopeana na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.Wengi wanamjua Zari kutokana na urembo wa kipekee aliojaliwa na mkwanja wa kufa mtu, akiwa anamiliki ndinga za bei mbaya zikiwemo Ranger Rover Sports 2014, BMW, Black Chrysler, Audi Q7, Silver Crysler 2008, Mercedes Benz Convertible na nyingine kibao, zote zikiwa na ‘plate number’ inayosomeka jina lake la Zari.
Hata hivyo, ni wachache wanaojua siri ya utajiri wa mwanadada huyo ambaye kiasili baba yake ana mchanganyiko wa Burundi na Somalia wakati mama yake ana mchanganyiko wa Mhindi na Mganda.
IVAN SSEMWANGA NDIYO KILA KITU
Kabla ya kuanza ‘projekti’ na Diamond, Zari alikuwa ameolewa na mfanyabiashara mkubwa wa Kiganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini, Ivan Ssemwanga ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea wachache kutoka Uganda, akiwa anaingiza faida ya zaidi ya shilingi za Uganda milioni 700 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 428 za Kibongo).
MALI ANAZOMILIKI IVAN
Achana na magari ya kifahari ambayo hayana idadi, yote yakiwa na ‘plate number’ yenye jina la Ivan, mchizi pia anamiliki Private Jet (ndege binafsi). Pia anamiliki utitiri wa vyuo vya Brooklyn City College, vikiwa na jumla ya ‘campus’ sita nchini Afrika Kusini katika Majiji ya Durban, Pretoria na Johannesburg, kila moja ikiwa na wanachuo kati ya 800 hadi 2100.
Watoto wa Zarinah Hassan, ‘Zari’.
Kozi zinazofundishwa kwenye vyuo vyake ni Information Technology
(IT), Mining (uchimbaji wa madini) na Policing (Sera za biashara) ambazo
zinapendwa na wengi Afrika Kusini, hali inayofanya apate wanachuo
kibao.Pia jamaa anamiliki bonge moja la mjengo lililopo Sir Apollo Kaggwa Road, Kampala pamoja na nyumba nyingine za kifahari zilizotapakaa maeneo ya Munyonyo, Bunga, Mutungo na Mukono nchini Uganda.
Pia jamaa anamiliki nyumba nyingine iliyopo Waterkloof Glen jijini Pretoria, Afrika Kusini na kuwa miongoni mwa Waganda wachache wanaomiliki nyumba nchini humo. Pia ana utitiri wa supermarkets, maduka ya vito vya thamani na maduka ya nguo (boutique) nchini Afrika Kusini.
KUFURU YA FEDHA
Hivi karibuni, Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes ilikuwa na mechi dhidi ya Timu ya Taifa ya Zambia (Chipolopolo) ambapo jamaa alifanya kufuru ya aina yake kwa kutoa shilingi milioni 10 za Uganda (zaidi ya shilingi milioni 6 za Kibongo) kwa kila mchezaji na kuahidi kutoa shilingi milioni 5 za Uganda (zaidi ya milioni 3) kwa kila atakayefunga bao.
Zarinah Hassan ‘Zari’, 'The Boss Lady' akipozi.
Kama hiyo haitoshi, jamaa alikodi helikopta iliyombeba yeye na
wapambe wake 10 aliosafiri nao kutoka Afrika Kusini na kuwalipia kila
kitu kuelekea kwenye Mji wa Namboole, Uganda kushuhudia mechi hiyo
ambayo hata hivyo Uganda haikushinda.AMETOKEA WAPI?
Ivan aliyezaliwa kwenye familia yenye uwezo wa kawaida, alisafiri kwenda Afrika Kusini akitokea Uganda mwaka 2002 kwa msaada wa mpwa wake, Kyeyune aliyekuwa akifanya biashara ya magari ya kifahari Bondeni.
Baada ya kukaa naye kwa kipindi kifupi, Ivan naye alianza kujishughulisha na biashara hiyo ambapo alifanikiwa kutusua kinoma. Maisha yake yakabadilika, akaanza kuwekeza kwenye biashara nyingine nyingi mpaka akawa bilionea. Vijana wengi wa Afrika Kusini wanamtambua kwa jina la Shaba Wa Shaba 9 kutokana na uwezo wake wa kifedha.
ANAMPAJE JEURI YA FEDHA?
Rekodi zinaonesha kwamba kabla Zari hajakutana na bilionea huyo, alikuwa mtu wa kawaida sana, akijishughulisha na mambo ya urembo na saluni za kike lakini walipokutana, kupendana kisha kuoana, ndipo mwanadada huyo alipoanza kushaini kwa kuendesha ndinga kali na hadhi ya maisha yake ikabadilika.
Pia inaelezwa kuwa hata baada ya uhusiano wao kwenda mrama, bado Ivan anaendelea kumhudumia Zari na watoto wake watatu waliozaa pamoja, Pinto, Didy na Quincy kwa kuwapa mkwanja mrefu mara kwa mara huku mwanamke huyo akisimamia miradi mingi ya mwanaume huyo ambaye inaelezwa kuwa licha ya kutengana, hawajapeana talaka.
Huyo ndiyo Ivan Ssemwanga, kidume anayempa jeuri ya fedha Zari!
0 comments:
Post a Comment