Wahamiaji 22, wengi wao watoto, wamekufa maji wakijaribu kufika visiwa vya Kalymnos na Rhodes nchini Ugiriki wakitokea Uturuki.
Huo ndio mkasa wa pili mkubwa kuhusisha wahamiaji wanaotaka kufika Ulaya katika visiwa hivyo vya Ugiriki.Maafisa wa serikali nchini Ugiriki wanasema watu 19 walifariki na wengine 138 wakaokolewa karibu na kisiwa cha Kalymnos.
Wengine watatu walifariki karibu na kisiwa cha Rhodes na wengine watatu hawajulikani waliko. Sita waliokolewa.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema amehuzunishwa na hatua ya Ulaya kutoangazia kikamilifu mkasa huo wa kibinadamu.
Akihutubu bungeni, kiongozi huyo wa chama cha Syriza ameshutumu “kiwango cha majadiliano katika ngazi ya juu, ambako mtu mmoja anmkabidhi mwenzake lawama” katika Muungano wa Ulaya (EU).
"Wanatoa machozi ya mamba kuhsu watoto wanaofariki katika fuo zetu kwa sababu watoto daima huibua huzuni, lakini wanafanya nini kuhusu watoto walio hai ambao wanafika hapa kwa maelfu na wanateseka katika kambi na misafara ya wahamiaji? Hakuna anayewajali,” amesema Bw Tsipras.
Hayo yakijiri, waokoaji kusini mwa Uhispania wanawatafuta wahamiaji 35 ambao hawajulikani waliko baada ya boti yao kuzama ikielekea Morocco. Miili minne imepatikana.
0 comments:
Post a Comment