Mwananamama
huyo anayeitwa Emma Moran raia wa Verbania Italy ametangazwa hivi
karibuni kuwa ni mtu mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani akiwa
na umri wa miaka 116.
Akitoa
sababu zake za kuishi muda mrefu zaidi amesema sababu kubwa ni kula
mayai mabichi na kutokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, jambo ambalo
limeshangaza watu wengi, imesemekana yeye ndiye anaweza kuwa mtu wa
mwisho aliyezaliwa karne ya 19 na kuishi mpaka leo karne ya 21.
Akiongea
na New York times mwaka 2015 alisema kuwa mayai hayo mabichi anakula
mara mbili kwa siku na pia alikuwa na wapenzi wengi hapo awali enzi za
usichana wake lakini baada ya kuingia kwenye ndoa isiyo na furaha kwake
aliachana na mumewe mwaka 1938 na hakuwahi kuolewa tena………
>>>”Sikutaka kutawaliwa na mtu yeyote na ndio kimenifanya niishi mpaka leo‘
Bibi huyo amekuwa mtu mwenye umri mrefu zaidi duniani baada ya Susannah Mushatt Jones kufariki siku ya May 12 2016.
0 comments:
Post a Comment