>>JUMAMOSI MTANANGE: BAYERN MUNICH v BORUSSIA DORTMUND!
Kocha Jurgen Klopp amekiri hali ni mbaya kwenye Timu yake ambayo Jumanne itacheza Ugenini na St. Pauli, Timu ya Daraja la Pili, kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Germany, DFB-Pokal.
Msimu huu, ngome kubwa ya Dortmund, Signal Iduna Park, imebomolewa mara 4 kwa kufungwa hapo hapo Uwanjani kwao kwenye Mechi za Bundesliga ambako wapo Nafasi ya 4 toka mkiani wakiwa na Pointi 7 tu, zikiwa ni Pointi 14 nyuma ya Vinara Bayern Munich.
Hali hii inashangaza hasa ukizingatia kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Kundi D wameshinda Mechi zao zote 3 kwa kuzitwanga Arsenal, Anderlecht na Galatasaray.
Huku Klopp akipigwa darubini kali inayotishia kibarua chake, Kocha huyo amekiri Wachezaji wake wamekumbwa na mchecheto ambao unaathiri uchezaji wao na hilo huchangia matokeo mabovu.
Akiongea hii Leo, Jurgen Klopp amefafanua: “Woga wa kutoshinda upo. Wakati mwingine tunakosa muda wa kupumzika kwa kukabiliwa na Mechi mfululizo lakini inabidi tufanye kazi.”
Pengine kitu kingine ambacho kimeiathiri Dortmund Msimu huu ni listi ndefu ya Majeruhi lakini Klopp amesema sasa wanapata afueni toka kwa hilo.
Kwenye Bundesliga, Mechi inayoafuata kwa BV Borussia Dortmund ni safari ya kwenda Allianz Arena Jumamosi ijayo kuwavaa Vinara na Mabingwa wa Bundesliga, Bayern Munich.
DFB-Pokal
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumanne Oktoba 28
21:00 DSC Arminia Bielefeld v Hertha Berlin
21:00 VFB Chemnitzer v SV Werder Bremen
21:00 Kickers Offenbach v Karlsruher SC
21:00 VfR Aalen v Hannover 96
22:30 FC Kaiserslautern v SpVgg Greuther Furth
22:30 MSV Duisburg v FC Koln
22:30 FC St. Pauli v BV Borussia Dortmund
22:30 FC Dynamo Dresden v VFL Bochum
Jumatano Oktoba 29
21:00 TSV 1860 Munich v SC Freiburg
21:00 FC Magdeburg v Bayer 04 Leverkusen
21:00 Wurzburger v Eintr. Braunschweig
21:00 RB Leipzig v FC Erzgebirge Aue
22:30 Hamburger SV v Bayern Munich
22:30 VfL Wolfsburg v Heidenheimer
22:30 Eintracht Frankfurt v Borussia Mönchengladbach
22:30 TSG Hoffenheim v FSV Frankfurt
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
BUNDESLIGA
RATIBA
**Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 31
2230 Schalke 04 v FC Augsburg
Jumamosi Novemba 1
1730 Hamburger SV v Bayer 04 Leverkusen
1730 Hannover 96 v Eintracht Frankfurt
1730 VfB Stuttgart v VfL Wolfsburg
1730 FSV Mainz 05 v SV Werder Bremen
2030 Bayern Munich v BV Borussia Dortmund
Jumapili Novemba 2
1730 Borussia Mönchengladbach v TSG Hoffenheim
1930 FC Koln v SC Freiburg
1930 SC Paderborn 07 v Hertha Berlin
0 comments:
Post a Comment