LEJENDARI
wa Cameroon Roger Milla ameshutumu mapendekezo ya Morocco ya kutaka
Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, ziahirishwe kuchezwa
Nchini mwao kutokana na mlipuko wa Ebola.
Fainali
hizo zitakazoshirikisha Nchi 16, wakiwemo Wenyeji Morocco, zimepangwa
kuanza Januari 17 lakini Morocco wameomba ziahirishwe kutokana na
mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola uliozikumba Nchi kadhaa huko Afrika
Magharibi na kuua Watu zaidi ya 4,400.
Lakini
Milla, Staa wa Cameroon alieng’ara mno kwenye Fainali za Kombe la Dunia
za Mwaka 1990, amesema Morocco inaficha kitu na Ebola ni kisingizio tu.
Milla,
akiongea Mjini Yaounde Juzi Jumatano, amesema: “Nimefuatilia hili na
najiuliza kwa nini Morocco ichukue hatua hii. Sidhani kama wanaogopa
Ebola. Nadhani wao wanaficha kitu. Bora wawe wa wazi tu.”
Vile
vile Roger Milla alihoji ikiwa CAF itahamisha Fainali hizo kutoka
Morocco Nchi hiyo itafanywa nini na kama Mwenyeji mpya atapewa nafasi ya
kushiriki moja kwa moja Fainali.
Msimamo
wa Roger Milla unafana na ule wa Mdadisi mmoja wa Soka ambae
ameshangazwa na jinsi AFCON 2015 kushinikizwa kuahirishwa kwa ajili ya
Ebola wakati Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani yanayotarajiwa
kuanza Nchini Morocco Desemba 10 na hakuna yeyote aliesema lolote.
Hivi
sasa AFCON 2015 ipo hatua ya Makundi ili kupata Nchi 15 ambazo
zitajumuika na Morocco kucheza Fainali na Mechi za Makundi zinatarajiwa
kumalizika Novemba 17.
Wakati
utata huu ukiendelea, CAF imedokezwa kuongea na Nchi kadhaa zikiwemo
Ghana na Afrika Kusini na Nchi nyingine 5 kuwa Wenyeji wa dharura ikiwa
Morocco watajitoa.
CAF wanatarajiwa kutoa msimamo wao baada kukutana na Morocco hapo Novemba 3.
CAF wanatarajiwa kutoa msimamo wao baada kukutana na Morocco hapo Novemba 3.
0 comments:
Post a Comment