RAIS
wa Mashujaa Band, Chaz Baba wiki iliyopita alichafua hali ya hewa
kwenye bendi yake baada ya kukwaruzana na viongozi wa ngazi za juu wa
bendi hiyo na baadae kutoonekana kwenye maonyesho yaliyosalia ya wiki
nzima.
Ilikuwa
ni katikati ya wiki kwenye ukumbi wa Flamingo Magomeni ambapo inadaiwa
Chaz Baba alichukizwa na kitendo cha Jado FFU aliyekuwa amesimamishwa,
kurudishwa kazini bila yeye rais wa bendi kujulishwa.
Saluti5 imeelezwa kuwa Chaz Baba ambaye alichelewa kufika ukumbini, alikuwa mbogo baada ya kukuta Jado FFU yupo mzigoni.
Ripota wa Saluti5 amedai mtafaruku ulikuwa mkubwa kiasi cha mashabiki wengi kubaini kuwa kuna ‘sintofahamu’ inayoendelea.
Baada
ya onyesho hilo, Chaz Baba hakuonekana tena kazini wiki hiyo, huku
wengine wakisema kasimamishwa kazi na wengine wakisema kajisimamisha
mwenyewe.
Hata
hivyo mmoja wa viongozi wa Mashujaa Band licha ya kukiri kuwa Chaz Baba
alikosa adabu, lakini akaweka wazi kuwa mwimbaji huyo hakusimamishwa.
Naye
Chaz Baba alipoulizwa na Saluti5 alisema hajasimamishwa wala
kujisimamisha bali hajaonekana kazini kufuatia kusumbuliwa na tumbo.
“Tumbo
lilikuwa linanisumbua nikashindwa kufika kazini kwa siku mbili tatu,
ila yaliyopita yamepita, wiki hii ntakuwepo kazini kama kawaida,”
alisema Chaz Baba kwa njia ya simu.
Kwa
wiki za hizi karibuni kumekuwa na ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya
wasanii wa Mashujaa Band na kupelekea baadhi ya yao kusimamishwa kazi.
Mbali na mwimbaji Jado, wasanii wengine waliokumbana na rungu la nidhamu, ni marapa Sauti ya Radi na Ferguson.
0 comments:
Post a Comment