Rais Michael Sata amefariki dunia. Mapema LEO asubuhi Katibu wa bunge la Zambia Rowland Msiska alithibitisha kifo cha rais Sata kilichotokea mjini London.
Sata aliye na miaka 77 aliondoka Zambia kuelekea jijini London zaidi ya wiki moja iliopita kwa matibabu ya ugonjwa ambao bado mpaka sasa haujawekwa wazi. Sata aliandamana na mke wake pamoja na watu wengine wa karibu wa familia yake. Kwa mujibu wa katibu Msiska, Rais Sata alifariki Jumanne jioni.Lakini vyombo vya habari awali vilikuwa vimeripoti Sata aliruhusiwa kutoka hospitali ili apate matibabu chumbani mwake huko nchini Uingereza. Rais huyo wa Zambia ameiongoza nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ya pili kwa ukubwa wa uzalishaji shaba tangu mwaka wa 2011.
0 comments:
Post a Comment