Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, October 17, 2014

HATIMAYE KESHO KUJUA MBIVU NA MBICHI KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM KATI YA WATANI WA JADI YANGA Vs.SIMBA



KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA 7,000/-
DABIYAKARIAKOO-19APR14Hapo kesho katika Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba itakayochezwa kesho Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro.

Lakini pia mashabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi ambayo ni kesho, Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki wa mechi hiyo  na itakuwa wazi kuanzia saa 4 asubuhi.
Pia magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. hivyo washabiki hawataruhusiwa kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa ikiwa lengo ni kuimarisha amani na usalama uwanjani hapo,pia Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.

Chanzo (TFF).................

0 comments: