Kocha wa Newcastle united Alan Pardew |
Gonjwa la Ebola limeikumba Afrika Magharibi na kuua Watu zaidi ya 4,000 na hivi sawa huko Uingereza Vituo vya Forodha vya Majini na kwenye Ndege Watu hupimwa Ugonjwa huo.
Sasa Klabu ya Newcastle nayo imeamua kuwapima Wachezaji wao Waafrika wanaorejea Klabuni baada ya kucheza Mechi za Kimataifa na Nchi zao.
Wachezaji wa Newcastle, Papiss Cisse, anaetoka Senegal, na Cheik Tiote, wa Ivory Coast, walikwenda Nchini mwao na pia kusafiri na Timu zao kucheza Mechi za Makundi za AFCON 2015 huko Tunisia na Congo DR.
Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, amekiri Klabu yao watakuwa wapuuzi ikiwa hawaukubali Ugonjwa huo.
: “Tunao mkakati wakirudi wao na Familia zao wataangaliwa. Hii ni kuwalinda na kuwasaidia.”alisema Pardew.
Lakini pia nchi 3 tayari zilishapigwa marufuku na CAF kucheza Mechi kwao baada ya kuvamiwa na Ugonjwa huu na hizo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone.
_________LIGI KUU ENGLAND
RATIBA-Mechi zijazo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 18
1445 Man City v Tottenham
1700 Arsenal v Hull
1700 Burnley v West Ham
1700 Crystal Palace v Chelsea
1700 Everton v Aston Villa
1700 Newcastle v Leicester
1700 Southampton v Sunderland
Jumapili Oktoba 19
1530 QPR v Liverpool
1800 Stoke v Swansea
Jumatatu Oktoba 20
2200 West Brom v Man United
0 comments:
Post a Comment