MANCHESTER CITY Jana Usiku walianza Ligi Kuu England kwa kishindo cha Ugenini huko The Hawthorns walipoitandika West Bromwich Albion Bao 3-0.
Hadi Mapumziko City walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zote zikifungwa na Yaya Toure.
Dakika
ya 9 Yaya Toure aliipa City Bao baada ya kupasiwa na Jesus Navas lakini
upo uwezekano Mpira huo uliparazwa pia na David Silva na kumbabatiza
Beki wa West Brom Craig Dawson na kumhadaa Kipa wao Boaz Myhill.
Bao
la pIli lilifungwa Dakika ya 24 kwa Shuti la juu la Toure na Kepteni
Vincent Kompany kupiga Bao la 3 Dakika ya 59 kwa Kichwa alipounganisha
Kona.
Dosari
pekee kwa Man City ambayo walitawala Mechi yote ni kulazimika kumtoa
Toure katika Dakika ya 80 akiwa na maumivu ya Nyonga na sasa upo
wasiwasi kama Jumapili atakuwa fiti kwa mtanange mkali huko Etihad dhidi
ya Mabingwa Chelsea.
Nae Mchezaji mpya wa City Raheem Sterling alichezea vizuri ingawa alipumzishwa Dakika ya 74 na kuingizwa Samir Nasri.
VIKOSI:
West Brom:Myhill,
Chester, Dawson, Lescott, Brunt, Morrison, Gardner, Fletcher, McClean
(Yacob - 45'), Lambert (Anichebe - 74'), Berahino (McManaman - 80')Akiba: Olsson, Yacob, Ideye, Anichebe, McManaman, Sessegnon, Rose.
Man City:Hart; Sagna, Kompany, Mangala, Kolarov; Toure (Demichelis - 80'), Fernandinho; Jesus Navas, Silva, Sterling (Nasri - 74'), Bony (Agüero - 63')
Akiba: Zabaleta, Nasri, Aguero, Caballero, Demichelis, Denayer, Iheanacho.
REFA: Mike Dean
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Agosti 8
Man United 1 Tottenham 0
Bournemouth 0 Aston Villa 1
Everton 2 Watford 2
Leicester 4 Sunderland 2
Norwich 1 Crystal Palace 3
Chelsea 2 Swansea City 2
Jumapili Agosti 9
Arsenal 0 West Ham 2
Newcastle 2 Southampton 2
Stoke 0 Liverpool 1
Jumatatu Agosti 10
West Brom 0 Man City 3
Ijumaa Agosti 14
2145 Aston Villa v Man United
Jumamosi Agosti 151445 Southampton v Everton
1700 Sunderland v Norwich
1700 Swansea v Newcastle
1700 Tottenham v Stoke
1700 Watford v West Brom
1700 West Ham v Leicester
Jumapili Agosti 16
1530 Crystal Palace v Arsenal
1800 Man City v Chelsea
Jumatatu Agosti 17
2200 Liverpool v Bournemouth
0 comments:
Post a Comment