Kitendo
cha kujaaliwa kupata mtoto wa kike, kimeonekana kumzuzua mwanamuziki
Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambapo sasa anadaiwa kushinda kutwa nzima
chumbani akipiga picha za kuposti mitandaoni.
Chanzo makini ambacho ni ndugu wa
Diamond kimeeleza kuwa, tangu jamaa huyo aitwe Baba Tiffah, amekuwa
akitumia muda mwingi na mwanaye huyo kiasi kwamba amepunguza hata kasi
ya kufanya muziki na kutokula.
“Jamaa ni kama kadata vile, yaani kuna
siku anashinda chumbani tu akimsaidia Zari kulea, ikiwa hivyo basi siku
hiyo itakuwa ni ya kupiga picha tu za kutupia mitandaoni, kiukweli mtoto
amemzuzua mshikaji,” kilidai chanzo hicho.
0 comments:
Post a Comment