Haijawahi kutokea. Siyo mabomu ya machozi wala polisi wenye silaha walioweza kuzuia halaiki ya wananchi kufika kwenye viwanja vya Furahisha kuhudhuria mkutano wa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Hii
ni kwa sababu umati uliojitokeza kuanzia Uwanja wa Ndege wa Mwanza
ambako polisi walilazimika kupiga mabomu yasiyohesabika kuwatawanya
wananchi ambao walifunga barabara inayoingia uwanjani hapo, kutozaa
matunda.
Msafara
wa Lowassa anayeungwa na mkono na vyama vinavyounda Ukawa vya Chadema,
NCCR-Mageuzi, NLD na Cuf, ulilisimamisha Jiji la Mwanza kwa takriban saa
tatu kutokana na msafara kutembea kilomita sifuri kwa saa.
Pamoja
na polisi kupiga mabomu mita chache kutoka uwanjani hapo, Lowassa
alipotoka tu uwanjani, umati mkubwa wa wafuasi wake na wa Ukawa,
waliokuwa wamejificha waliibuka wakiwa na chupa za maji; mbele ya askari
waliokuwa kwenye magari wakiwa na silaha za moto na mabomu ya machozi.
Kilichochangia
msafara kutembea mwendo mdogo ni baadhi yao kumwaga maji barabarani
kama ishara ya kupiga deki ili Lowassa apite huku wengine waliokuwa na
fagio za chelewa, wakifagia.
Wananchi wengine walikuwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ikiwamo ‘Richmond ilikuwa ni maagizo ya juu’; ‘pombe mwisho kaunta, Ikulu ni Lowassa’; ‘kufuli mwisho mlangoni’; na ‘Tanzania bila Lowassa haiwezekani.’
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, akizungumza na waandishi wa
habari uwanjani hapo, alisema polisi hawajawazuia wananchi kushiriki
mkutano bali wamepiga mabomu kuzuia wale ambao wamekwenda uwanja wa
ndege ambako siyo eneo la mkutano.
“Hatuna
nia ya kuzuia mkutano, wananchi tumewaambia kwamba waende Furahisha kwa
sababu wakija huku watasababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa
uwanja,” alisema.
Ikiwa
uwanjani hapo, Mpekuzi ilisikia milipuko ya mabomu zaidi ya 30
yaliyopigwa kwa takriban saa moja kabla msafara wa Lowassa haujaondoka
kuelekea Furahisha.
Tofauti
na mikoa mingine, maandamano ya Mwanza hayakuwa na pikipiki, bajaj wala
magari zaidi ya yale ya viongozi wa Ukawa taifa na wabunge wa Chadema
kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, bali ni wananchi wasiohesabika ambao
walilazimisha mkutano kutembea kilomita sifuri kwa saa.
Idadi
ya watu waliojitokeza kwenye uwanja wa Furahisha, nusura usababishe
mkutano kuahirishwa baada ya watu kuanza kuzimia na kupoteza fahamu,
jambo ambalo lilisababisha kikosi cha Msalaba Mwekundu uwanjani kuzidiwa
nguvu.
Kutokana
na hali hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwaambia
wananchi warudi nyuma na wengine wakae chini ili kutoa nafasi kwa
viongozi, waandishi na wapigapicha wafanya kazi yao.
Hata
hivyo, tangazo hilo halikufua dafu kwani baadhi ya wananchi waliokuwa
mbele, walikaa chini lakini halaiki hiyo iliendelea kusababisha usumbufu
mkubwa kutokana na idadi ya watu walioendelea kupoteza fahamu.
Baada
ya kuanza kusukumana, wananchi wengine walianza kulia na kusema kuwa
walilala uwanjani kumsubiri Lowassa na viongozi wa Ukawa, lakini
wanasikitika kusukumwa na kukanyagwa.
0 comments:
Post a Comment