Timu
ya taifa ya Algeria ndiyo timu ya kwanza kujikatia tikiti ya kushiriki
dimba la kombe la Afrika hapo Januari mwaka ujao baada ya kuinyuka timu
ya taifa ya Malawi mabao 3-0.
Riyad Mahrez anayeichezea klabu ya Leicester city katika ligi ya Uingereza, aliongeza bao la pila katika kipindi cha pili, hii ni baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Sofiane Feghouli na kufunga kwa urahisi kabisa.
Mahrez aliendelea kung'ara na baadaye kutoa pasi safi ya juu iliyokamilishwa na kichwa na Slimani na kumuacha mlinda lango hoi na kufunga bao la tatu na la mwisho huku wakiisaidia Algeria kujipatia nafasi ya kushiriki dimba la kombe la taifa bingwa Afrika
0 comments:
Post a Comment