Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Thursday, October 16, 2014

STEPHEN KESHI APATA MRITHI NIGERIA

shaibu Amodu

Shirikisho La kandanda la Nigeria NFF limefichua kwamba Shaibu Amodu ndiye atakayechukua nafasi ya Stephen Keshi kama mkufunzi wa timu ya taifa ya Nigeria.

Hatua hii imechukuliwa muda mfupi tu baada ya bw. Keshi kuiongoza Nigeria katika mechi waliyoshinda kwa mabao 3-0 ingawa hakuwa amepatiwa mkataba na kufufua matumaini ya Nigeria ya kufuzu kwa dimba la kombe la Afrika litakaloandaliwa huko Morocco mwaka ujao
.
Baada ya kufanya mkutano wa dharura, shirikisho la kandanda nchini Nigeria limeamua kumteua Amodu kuingoza timu ya taifa ya Nigeria katika mechi zake mbili zitakazochezwa hapo Novemba katika juhudi zao za kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Afrika.
Hata hivyo wamesema mkufunzi wa kudumu kutoka nchi za kigeni ataajiriwa baadaye.
stephen keshi
Amodu anakabiliwa na wakati mgumu kwani lazima ashinde mechi zote mbili watakazocheza ambapo mechi moja watakuwa wageni wa timu ya taifa ya Jamhuri ya kidemokrasia ya congo huku ya pili wakiwa wenyeji wa timu ya taifa ya Afrika kusini endapo watafuzu.

Aidha mabingwa hao wa bara la Afrika wapo katika hatari kubwa ya kutofuzu na kushindwa kutetea taji lao.
Ushindi walioupata dhidi ya Sudan ndio uliokuwa wao wa kwanza katika kundi A na kuisaidia kupanda ngazi kutoka mwisho. Kwa sasa wako pointi tatu nyuma ya Congo ambao wanashikilia nafasi ya pili.

"Kamati tendaji imefanya uamuzi wa kumuachilia Keshi aondoke na kumpa Shaibu Amodu mamlaka ya kuiongoza Nigeria katika mechi zake mbili zijazo," msemaji wa NFF Ademola Olajire ameiambia BBC

0 comments: