Kundi la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi mara kwa mara katika mji wa Potiskum |
Shambulizi lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.
Shule hiyo ni ya mafunzo ya sayansi. Mwalimu mmoja alinukuliwa akisema kuwa alisikia mlio mkubwa wa kutisha wakati bomu hilo lilipolipuka.
Kadhalika kundi hilo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5 likitaka kuunda dola ya kiisilamu huku likipinga elimu ya kimagharibi.
Wiki jana shambulizi la kujitoa mhanga lilifanyika mjini humo na kuwaua watu 15 wakati wa maandamano ya kidini.
0 comments:
Post a Comment