Madaktari
wa Australia wamefanikiwa kuwarejeshea uhai wagonjwa watatu baada ya
kupandikizwa moyo uliokufa katika operesheni ya kwanza kufanyika
duniani.
Madaktari katika hospitali ya St Vincent mjini Sydney walitumia dawa ya kuzuia kuharibika iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti wa Moyo ya Victor Chang kwa kupandikiza viungo kwa Michelle Gribilas,mwenye umri wa miaka 57 na Jan Damen mwenye umri wa miaka 44, huku mgonjwa wa tatu akiendelea kupona.
Moyo mmoja, ulisimama mapigo kwa dakika 20 kabla ya kuurejesha katika uhai, ukiwa umewekwa katika mashine na kuuchoma dawa ya kuzuia kuharibika.
Wagonjwa wawili waliopandikizwa moyo (Michelle Gribilas, kushoto, na Bwana Damen, katikati) wanazungumza na daktari wa upasuaji Kumud Dhital
Moyo unahuishwa baada ya kupoteza uhai na kupandikizwa. Hospitali hiyo inaamini asilimia 30 za watu watarejeshewa uhai kutokana na kugunduliwa kwa dawa hii, ambayo hupunguza kiwango cha uharibifu kwenye moyo na kuwa tayari kupandikizwa.
Dawa hiyo iliyochukua miaka 12 kuitengeneza, pia inasaidia kuimarisha kazi ya moyo ambao unatolewa baada ya kifo (DCD) wakati ukianzishwa kufanya kazi upya.
Bi Gribilas, ambaye amestaafu na kuishi Campsie kusini magharibi mwa Sydney, amesema ni mtu tofauti kwa sasa baada ya kupandikizwa moyo mpya.
0 comments:
Post a Comment