Kilabu
ya taifa la Ugiriki Pas Lamia kimemtaka mchezaji wake kutoka Sierra
Leone John Kamara kutofanya mazoezi ama hata kuichezea kilabu hiyo kwa
mda wa wiki tatu kutokana na hofu za ugonjwa wa Ebola.
''kilabu hiyo imeniambia kwamba sifai kuwa na timu hiyo kwa muda wa siku 15 hadi 21 kwa kuwa nilienda barani Afrika kucheza na kwa sababu ya virusi vya ugonjwa wa Ebola'',Kamara aliiambia BBC.
''Wameniambia wazi kwamba ninafaa kukaa nyumbani ama naweza kusafiri kwenda ughaibuni kuiona familia yangu lakini si kufanya mazoezi na kilabu hiyo''
.
Sierra Leone ililazimika kuandaa mechi yake dhidi ya Cameroon mjini Younde kwa kuwa imepigwa marufuku kuchezea nyumbani na shirikisho la soka barani Afrika kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Hatua hiyo ya kilabu ya Lamia inajiri licha kuwa hakuna kisa chochote cha Ebola kilichoripotiwa nchini Cameroon na kwamba Mchezaji huyo hajasafri kwenda Sierra Leone kwa takriban mwaka mmoja sasa.
0 comments:
Post a Comment