Sturridge akipokea maelekezo fulani kutoka kwa kocha wake, Brendan Rodgers katika moja ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza 2014/2015 |
Tangu
Sept 3, 2014, mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge amekuwa nje
ya dimba kwa sababu ya maumivu ya misuli ya paja (thigh injury)
yaliyokuwa yakimsumbua ambayo aliyapata wakati akichezea timu yake ya
taifa ya Uingereza dhidi ya Norway, mchezo ambao ulimalizika kwa
Uingereza kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Baada
ya kukaa nje ya dimba kwa takribani wiki mbili akiuguza jeraha lake
hilo, hivi karibuni Sturridge alirudi uwanjani kuungana na wachezaji
wenzake wa Liverpool katika kambi ya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na
michezo migine ya ligi kuu ambapo alipata jeraha ligine la misuli ya
mguu (calf injury).
"Tulikuwa
tunategemea Daniel Sturridge atarudi uwanjani kuanzia Jumapili Oct 19,
2014 wakati tukicheza dhidi ya Queens Park Rangers, lakini sidhani kama
tutakuwa naye kwa sababu tayari anasumbuliwa na misuli ya miguu kwa mara
nyingine tena," Hiyo ni kauli yake kocha wa Liverpool Brendan Rodgers
akizungumza na waaandisha wa habari jana.
Taarifa zinasema kwamba Daniel Sturridge atakuwa nje ya uwanja kwa muda mwezi mmoja akiuguza majeraha yake hayo.
0 comments:
Post a Comment