Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, January 18, 2016

Tanzia: Mtunzi wa Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe Afariki Dunia

IMG_20160117_234416


















Dk. Edwin Semzaba enzi za uhai wake.
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwandishi wa tamthiliya ya “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe,” Dk. Edwin Semzaba amefariki dunia jana  January 17, majira ya jioni.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya marehemu inasema kuwa, Dk. Semzaba amefariki dunia akiwa amelazwa hospitalini lakini familia hiyo hawajaweka wazi nini chanzo cha kifo cha mtunzi huyo mahiri wa vitabu tanzania.
Dk. Semzaba pia alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa  Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA ).
Jamii ya Watanzania itamkumbuka sana Dk. Edwin Semzaba kwa umahiri wake wa utunzi wa vitabu hasa kitabu cha “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe” ambacho kilisomwa sana na mpaka sasa kinatumika sana katika kufundishia wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini.

Related Posts:

0 comments: