Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi. PICHA|MAKTABA |
Badala yake, Sefue amemteua Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava kukaimu nafasi ya Maswi hadi
uchunguzi husika utakapokamilika.
Maswi (pichani), anakuwa kiongozi wa tatu kukumbwa
na dhoruba inayotokana na sakata la Escrow baada ya kujiuzulu kwa
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema na kung’olewa kwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
juzi.
Hatua ya Balozi Sefue inafanana na ile iliyowahi
kuchukuliwa na mtangulizi wake, Philemon Luhanjo Julai 21, 2011 pale
alipomsimamisha kazi kwa muda aliyekuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo,
David Jairo na kukaimisha nafasi yake kwa Maswi ili kupisha uchunguzi.
Baadaye Jairo alirejeshwa kazini lakini siku moja
baadaye Rais Kikwete alimrejesha nyumbani kutokana na shinikizo la
wabunge na tangu hapo hakuwahi kurudi katika utumishi wa umma na badala
yake Maswi alithibitishwa kuwa katibu mkuu hadi jana.
Hatua ya kusimamishwa kwa Maswi imekuja siku moja
tangu Rais Jakaya Kikwete alipoelekeza mamlaka za utumishi kuchukua
hatua dhidi ya Maswi baada ya kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma
zinazomkabili.
“Kuhusu katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, kwa vile ni mtumishi wa umma, anatawaliwa na sheria na kanuni za
utumishi wa umma, hivyo nimeshaelekeza mamlaka kuchunguza tuhuma zake
na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa,”
alisema Rais Kikwete wakati akilihutubia Taifa kupitia wazee wa Mkoa wa
Dar es Salaam juzi.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu jana, ilisema Balozi Sefue amechukua hatua hiyo kwa kutumia
madaraka aliyonayo kama mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa umma
wanaoteuliwa na Rais, wakiwamo makatibu wakuu.
Amechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Namba 8 ya 2002 (kama ilivyorekebishwa).
Maswi na watumishi wengine wa umma ambao wametajwa
watashughulikiwa na Tume ya Maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
Rushwa (Takukuru) pamoja na Jeshi la Polisi na ikithibitika kuwa
walikiuka maadili yao ya kazi, sheria stahiki zitachukuliwa.
Taratibu za uchunguzi
Kwa mujibu wa taratibu, Maswi analazimika kwenda
likizo kuanzia leo ili kupisha uchunguzi wa awali ambao unalenga kubaini
iwapo ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zinazoongoza
utumishi wa umma. Kwa kawaida likizo yake ni ya malipo.
Ikiwa uchunguzi wa awali utabaini kwamba ana makosa ya kinidhamu, atapewa taarifa za tuhuma husika ambayo itaambatana na hati ya mashtaka, ambayo itaeleza kwa kifupi makosa hayo na jinsi yalivyotendekea.
Ikiwa uchunguzi wa awali utabaini kwamba ana makosa ya kinidhamu, atapewa taarifa za tuhuma husika ambayo itaambatana na hati ya mashtaka, ambayo itaeleza kwa kifupi makosa hayo na jinsi yalivyotendekea.
Matokeo ya mchakato huo wa kinidhamu unaweza kuwa
kushushwa cheo, kupunguzwa mshahara, kufukuzwa kazi, kuachishwa kazi au
kurejeshwa kazini kutegemea matokeo ya taratibu zitakazofuatwa.
Kwa mujibu wa taratibu hizo, taarifa ya tuhuma itatoa maelezo kuhusu lini mtuhumiwa anapaswa awe amezijibu.
Baada ya kupelekewa atalazimika kujibu kwa
kuzikubali au kuzikataa na ikiwa atazikubali mamlaka ya nidhamu inaweza
kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Kama atakana au kukataa tuhuma husika, mamlaka ya
nidhamu inapaswa kuunda kamati ya uchunguzi ambayo itapewa muda maalumu
wa uchunguzi wa kuwasilisha tarifa yake kwa mamlaka ya nidhamu ikiwa ni
mapedekezo na Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kutoa adhabu kwa kuzingatia
mapendekezo hayo.
Mamlaka ya nidhamu baada ya kupitia mapendekezo
husika inawajibika kuendelea na mchakato wa kutoa adhabu kwa mujibu wa
Sheria ya Umma na kanuni zake na iwapo adhabu ni kuvuliwa madaraka,
mamlaka ya nidhamu italazimika kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi ambaye
ni Rais.
Ikiwa mtuhumiwa hataridhika na adhabu aliyopewa, taratibu zinampa fursa ya kukata rufaa kwa Rais.
source:mwananchi
source:mwananchi
0 comments:
Post a Comment