Barca walimuanzisha Straika wao mpya Luis Suarez ambae amemaliza Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada ya kumng’ata Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini.
Suarez ndie alietoa pasi iliyomfikia Neymar na kuihadaa ngome ya Real na kufunga Bao kiakili katika Dakika ya 4 tu.
Real walisawazisha Dakika ya 35 kwa Penati ya Cristiano Ronaldo iliyotolewa kufuatia Gerard Pique kuunawa Mpira na Dakika ya 50 kuongoza kwa Bao la Kichwa cha Pepe baada ya Kona.
Karim Benzema alipiga msumari wa mwisho kufuatia kaunta ataki alipolishwa na Ronaldo na kuandika Bao la 3 Dakika ya 61.
Real wangeweza kuongeza Bao kadhaa zaidi kama umaliziaji wao ungekuwa makini zaidi.
+++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Real Madrid 3
-Dakika ya 35 Cristiano Ronaldo [Penalti]
-50 Képler Laveran Pepe
-61 Karim Benzema
FC Barcelona 1
-4 Neymar Da Silva
+++++++++++++++++++++++++++
Hii ni Mechi ya kwanza kwa Barca kwenye La Liga Msimu huu kufungwa na pia ni mara ya kwanza kufungwa Mabao baada ya kushinda Mechi zao 7 na Sare 1 bila kutobolewa hata mara moja.
Matokeo haya yamewaweka Real Nafasi ya Pili wakiwa Poniti 1 nyuma ya FC Barcelona.
VIKOSI:
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Rodriguez, Modric (Arbeloa - 89'), Kroos, Isco (Illarramendi - 84'), Benzema (Khedira - 87'), Ronaldo.
Barcelona: Bravo, Alves, Pique, Mascherano, Mathieu, Xavi (Rakitic - 60'), Busquets, Iniesta (Sergi - 72'), Suarez (Pedro - 69'), Messi, Neymar.
REFA: Jesús Gil Manzano
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
FC Barcelona |
9 |
7 |
1 |
1 |
23 |
3 |
20 |
22 |
3 |
Real Madrid CF |
9 |
7 |
0 |
2 |
33 |
10 |
23 |
21 |
2 |
Sevilla FC |
8 |
6 |
1 |
1 |
15 |
8 |
7 |
19 |
4 |
Valencia |
8 |
5 |
2 |
1 |
17 |
7 |
10 |
17 |
5 |
Atletico de Madrid |
8 |
5 |
2 |
1 |
14 |
7 |
7 |
17 |
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Ijumaa Oktoba 24
Celta de Vigo 3 Levante 0
Jumamosi Oktoba 25
UD Almeria 0 Athletic de Bilbao 1
Real Madrid CF 3 FC Barcelona 1
2100 Valencia v Elche CF
2300 SD Eibar v Granada CF
2300 Cordoba v Real Sociedad
Jumamosi Oktoba 25
1400 Malaga CF v Rayo Vallecano
1900 RCD Espanyol v Deportivo La Coruna
2100 Sevilla FC v Villarreal CF
2300 Getafe CF v Atletico de Madrid
HISANI:SOKA IN BONGO
0 comments:
Post a Comment