Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Sunday, February 15, 2015

MAKALA:MWANAMKE UKIACHWA NA MPENZI WAKO FANYA HAYA


1.USIINGIE KATIKA UHUSIANO MWINGINE GHAFLA
Wapo wanaojikuta wakianzisha uhusiano mengine ghala bila kutulia. Kipindi hiki siyo cha kuanzisha uhusiano mwengine. Inashauriwa kutulia kwanza na kutafakari
kabla ya kuanzisha uhusiano mwingine kwani kwa kuharakisha unaweza kujikuta unaingia katika uhusiano ambao utakutesa maisha yako yote.
2. JITAMBUE KUWA WEWE NI MZURI
Mwanamke kwanza unatakiwa ujitambue wewe ni mzuri haijalishi kuwa utakuwa na pua ndogo au ndefu au una umbo baya lazima ndani yako kuna kitu kinakufanya uonekane mzuri tena ikiwezekana zaidi ya hivyo ukianzia kwenye macho, tabasamu lako, sauti na jinsi unavyocheka hivi na moyo wako wa ukarimu hivi ni vichache ambavyo hukufanya kujiona wewe ni mama, dada au binti mrembo.
3. JIFUNZE KUSEMA ASANTE
Unapokutana na mwanamume au mwanamke mwenzako barabarani, baa au sehemu ya starehe na akakwambia umependeza jifunze kusema asante huku ukiwa unatabasabu.
Mara nyingi wanawake wamekuwa wakiambiwa ‘umependeza’ badala kusema asante huanza kujiuliza na hii pua yangu ilivyokubwa, maungo yangu mabaya...Wengi hupenda kujieleza kimoyomoyo kutokana na kutojiamini. Pia, hata wanawake wengi ofisini huwa na tabia hii. Hivyo yakupasa kukubali sifa uliyopewa.
4. JIFUNZE KUSEMA HAPANA LAKINI ASANTE
Kipindi hiki pia wanaume au wanawake wenzako huvutiwa na wewe katika kukaa na kuongea kutoka kula chakula cha usiku. Hii haimaanishi huyo mwanaume anataka kulala na wewe hapana na siyo kosa kukataa kukataa ofa ya kinywaji na kuwa mkali kwa hiyo aliyekualika jiangalie mwenyewe kama unapendezwa na hicho kitu umwambia Hapana na asante kwa ofa.
5. KUFANYA MAPENZI HAKUMAANISHI UNAPENDWA
Image result for CRY BLACK WOMANMara nyingi mtu akifanya mapenzi hufikiria kwamba anapenda au anapendwa au wengine akishaaachwa husema sitaki kufanya mapenzi au mimi sisikii raha tena ya kufanya mapenzi. Hili ni kosa ambalo wanawake wengi hufanya.
Kama utataka fanya na yul
e mtu uliyemridhia kama hutaki sema hapana.
6. JIFUNZE KULALA VIZURI
Kutokana na kuzoea kulala wawili mara nyingi hujisikia kulala pembeni, mara katikati ili mradi kitanda ukiona kikubwa kutokana na hivyo jifunze kulala mapema na vizuri sababu hicho ni kitanda chako unatakiwa kulala.
7. JIFUNZE KUFANYA VITU PEKE YAKO
Mara nyingi umezoea kutoka wawili mfano kwenda bar, kanisani na kusafili hivi vyote ulizoea kufanya mkiwa wawili sasa jifunze kwenda na marafiki au peke yako ukishindwa toka mwenyewe na ujiamini bila kufikiria watu watakuonaje.
8. JIFUNZE KUSIMA KWA MIGUU YAKO MIWILI
Hii haimaanishi kwa miguu, ni kwamba baadhi ya wanawake ni mama wa nyumbani, hivyo alikuwa akifanya baba kama vile utafutaji fedha mfano matumizi ya nyumbani, ada za watoto, nguo na vitu vingine hivyo unatakiwa kujishughulisha na kuwa mjasiriamali hii itakusaidia sana kuendesha maisha yako na watoto wako. Pia, kwa mfanyakazi au mjasiriamali unatakiwa ufanye kazi kwa bidii.
9. JIFUNZE KUJIPENDA MWENYEWE
Mara nyingi wanawake ambao hawajaolewa hupatwa na mshawasha wa kuingia kwenye uhusiano mwingine haraka. Hivyo unashauriwa kusubiri kwanza jipe muda wa kuwa peke yako kwanza. Jifunze wapi ulikosea na ulipopatia kukimbilia kwenye uhusiano mwingine hukufanya kutomuelewa huyo unayeanza nae uhusiano na hukupelekea kurudia kosa lilelile.
Wengine utumie muda huu kumwomba mwenyezi Mungu akupe mume yule mnaendana nae
.  
10.MPE NAFASI MTU MWENGINE
Kuna wanawake wakisha talikiwa huona ndiyo mwisho wa wao kuwa na uhusiano mwengine, wengine wanafikia hata hatua ya kusema kuwa hatapenda tena. Hiyo siyo kweli. Una haki zote za kuwa na mwenza wako ili mradi umejipa nafasi na siyo kuingia katika uhusiano mapya kwa ghafla au kwa hasira.

0 comments: