Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya
CCM , mjini Unguja , Zanzibar jana. Kushoto ni Makamu wake (Zanzibar),
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein .
Kinana aliyasema hayo jana mjini hapa kuhusu mambo
yaliyojitokeza kwa wagombea wa nafasi za urais kabla ya kufanyika kwa
Uchaguzi Mkuu, Oktoba.
Kamati Kuu ya CCM hadi jana jioni ilikuwa ikiendelea na kikao chake kwenye ofisi kuu ya chama, Kisiwandui, Zanzibar.
Kauli ya Kinana imekuja baada ya kuwapo kwa
minong’ono kuwa baadhi ya makada waliojitokeza kutangaza ama kuonyesha
nia kuutaka urais watachukuliwa hatua, zikiwamo kutimuliwa.
“Mambo yanayozungumzwa ni mengi kuwa baadhi ya
wagombea majina yao yatakatwa. Hayo ni majungu ya kisiasa, yamelenga
kuwachokoza viongozi na chama ili wapate cha kusema.
“Chama kina utaratibu na uamuzi unaofanyika kwa vikao maalumu, hizi ni propaganda, ni uchokozi kwa chama chetu,” alisema Kinana.
0 comments:
Post a Comment