MKAZI wa Ilala Mtaa wa Lindi, Hafidhi Ally (23), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kuvamia kisha kuingia nyumbani kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Mbele
ya Hakimu Ester Kihiyo, karani wa mahakama hiyo, Mosses Mchome, alidai
kwamba mtuhumiwa alifanya kosa hilo Desemba 10, mwaka huu saa 7:30 usiku
nyumbani kwa Mzee Mwinyi, Mikocheni B, Dar es Salaam.
Karani
Mchome aliiambia mahakama hiyo kwamba, Hafidhi aliingia hadi ndani ya
nyumba hiyo bila ruksa kutoka kwa mlinzi aliyekuwapo kwenye lindo, Nuru
Saidi, ambapo alimweleza kwamba hana mahali pa kuishi.
“Mtuhumiwa
ulikaidi amri ya mlinzi aliyekuwepo zamu siku hiyo, aliyekutaka urudi
ulipotoka, kisha ulisisitiza kwamba huna sehemu ya kuishi, lakini pia
wewe ni mtoto wa rais huyo mstaafu wakati huo ukielekea ndani kitu
ambacho ni kinyume cha sheria,” alidai Mchome.
Mtuhumiwa alikana kosa hilo na upelelezi bado unaendelea.
Kesi
hiyo imeahirishwa hadi Desemba 28, mwaka huu na mtuhumiwa alirejeshwa
mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo
alitakiwa apeleke wadhamini wawili waaminifu wenye barua kutoka kwa
ofisa mtendaji wa kata anakoishi.
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment