Kenji Goto |
Japan imeelezea ghadhabu yake kwa kundi la wanamgambo la Islamic State ambalo limetoa kanda ya video inayoonyesha mauaji ya mateka raia wa nchi hiyo Kenji Goto.
Japan imeyataja mauaji hao kuwa kitendo cha kikatili ambapo waziri mkuu wa Japan mwenye hasira amesema kuwa japan itaendela kushirikiana na nchi zinazopambana na kundi hilo.Wiki moja iliyopita mateka mwingine raia wa Japan Haruna Yukawa aliuawa na wanamgambo hao.
Kenji Goto ambaye ni mwandishi wa habari alitekwa nyara nchini Syria mwezi Oktoba mwaka uliopita.
0 comments:
Post a Comment