
IMEFICHUKA! Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo
Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni
alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim
‘Sandra’, Sinza-Mori jijini Dar.
Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’
kuwa, Zari alipata fursa ya kupiga ‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea
Diamond.
“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu
wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya
Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.
“Awali, Diamond alitaka akamlaze hotelini lakini mtoto wa kike akakataa,
akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe, Diamond akasema
ruksa mama,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki
kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa
wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi
zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na 'Diamond Platnumz'.
“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
ALIPOTAFUTWA mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini
mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo
hazikutajwa.
0 comments:
Post a Comment