Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Itaendelea kutimua vumbi nchini Guinea ya Ikweta, ambapo timu za kundi D zitashuka dimbani kuwania pointi tatu muhimu.
Kiungo wa Ivory Coast Yaya toure ambaye alikua majeruhi anatarajiwa kucheza mchezo huo baada ya Kocha wake Herve Renard kueleza kuwa Yaya anaendelea vizuri.
Mchezo mwingine utakua ni kati ya Mali na Cameroon ambao nao utapigwa Estadio de Malabo
Cameroon wanatarajia kumtumia nahodha wake Stephane Mbia ambae alikua anatumikia adhabu toka mwezi Novemba alikotolewa kwenye mchezo dhidi ya Ivory Coast.
Mali itamkosa mshambuliaji wake Cheick Diabate ambae alifanyiwa upasuaji mapema Mwezi huu, huku kiungo wa Mali Seydou Keita akijiandaa kucheza michuano hiyo kwa mara ya saba katika kipindi chake cha uchezaji
0 comments:
Post a Comment