Polisi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wamefyatua risasi hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji mkuu Kinshasa kupinga sheria mpya ya uchaguzi.
Wanafunzi wameweka vizuizi barabarani na pia wameshuhjudiwa wakichoma magurudumu, katika barabara zinazoelekea katika chuo kikuu mjini humo.
Vurugu hizi zinashuhudiwa huku baraza la Senate likidadisi mswada ambao huenda ukasababisha Rais Kabila kuongezwa muda mamlakani.
Wanafunzi waliambia BBC kuwa polisi walivamia chuo chao baada ya wao kuanza kuandamana.
Walisema polisi walingia katika vyumba vyao na kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi.
Viongozi wa upinzani walitoa wito kwa waandamanaji kwenda barabarani kupinga mipango ya serikali kumuongeza muda zaidi mamlakani Rais Joseph Kabila huku wakiutaja mpango huo kuwa mapinduzi ya kikatiba.
Mswada huo unapendekeza kufanytika sensa kote nchini ambayo itachukua kipindi cha miaka mitatu.
Rais Kabila amekuwa mamlakani tangu mwaka 2001. Muhula wake wa pili unakamilika mwaka 2016 kikatiba.
0 comments:
Post a Comment