Chama cha watu wasioona mkoa wa Iringa waliopo katika wilaya ya kilolo wamewasihi wananchi
pamoja na wadau mbalimbali kuwaonesha ushirikiano katika shughuli za
kimaendeleo.
Akizungumuza na blog hii leo mwenyekiti wa
chama cha wasioona wilayani kilolo BI.Rusi Kisumbe alisema kuwa mara nyingi wamekuwa
hawathaminiwi katika jamii na kuonekana kama ni watu ambao
hawawaezi kufanya kitu chochote katika hususani katika shughuli
mbalimbali za kimaendeleo.
Mwenyekiti wa chama cha wasioona Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa Bi.Rusi Kisumbe akiwa na mjumbe wa chama hicho Bw.Haruna Makete. |
Aidha Bi. Kisumbe alisema, wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali kama vile kukosa ofisi za kuendeshea shughuli zao za kila
siku, ubovu wa mazingira wanayoishi, ikiwa ni pamoja na kutopewa mikopo ambayo
itawasaidi kujiendesha wenyewe kama chama.
Kwa upande wake mwanachama na mjumbe mtendaji wa chama hicho
cha wasioona wilayani kilolo Bw. Haruna Maketa nae alielezea changamoto kubwa ambayo wao
wanayokutana nayo ni kutokupewa fursa za kutosha katika umiliki wa ardhi tatizo jambo linawakwamisha hasa kwenye suala la kilimo.
Hata hivyo Bi. Kisumbe aliwataka wadau kuwasaidia
chama cha wasioona katika wilaya ya kilolo kwa kuwasaidia kwenye chama hicho ili kiweze kuendesha shughuli za kimaendeleo na kuwataka wanajamii kutowachukulia wao kama ni ombaomba kwa kuwa wao ni walemavu.
0 comments:
Post a Comment