Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Tuesday, October 14, 2014

BONANZA LA KUMUENZI BABA WA TAIFA LEO SAMORA

Leo katika kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa la Tanzania  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanamichezo  wameiadhimisha hii siku kwa kufanya baadhi ya michezo mbalimbali ya kumuenzi mwalimu Nyerere, michezo amabyo imefanyika kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa  na miongoni mwao ni Timu ya Maveterani wa Iringa ambao wamefanya michezo hiyo ya mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kualika timu mbalimbali katika kushiriki michuano hiyo kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa.


Lisa Mwalupindi  ambaye ni Captain wa timu ya Maveterani wa Iringa.
Miongoni mwa timu mbalimbali zilizoshiriki kwenye bonanza hilo la kumuenzi baba wa Taifa (Nyerere Day)ni timu ya Maveterani wa Iringa ambao walichuana vikali  na Maveterani wa Mkwawa na hatimaye Maveterani wa Iringa kuibuka na ushindi wa bao moja kwa nunge bao ambalo lilitiwa kimyani na mchezaji wa timu hiyo anayeitwa Baraka mnamo dakika ya kumi na tatu ya mchezo huo katika kipindi cha kwanza,uliofanyika kwenye uwanja wa samora mjini Iringa.

Kwa upande wake kocha huyo wa timu ya Mkwawa Veterani Bw. Dudu Haruna ambaye alielezea sababu ya kushidwa katika mchezo huo dhidi ya Maveterani wenzake wa Iringa,na kusema kuwa wao walikuwa na muda mchache sana katika kipindi  cha  kufanya mazoezi,lakini pia aliwalaumu baadhi ya wachezaji wake kwa kudai kuwa hawakuwa makini kwenye mchezo huo jambo ambalo limewafanya kutoshinda mchezo huo,alikiri wazi kuwa wachezaji wa timu pinzani walijiandaa vizuri na kutumia nafasi waliyoipata katika kuwafunga  wao bao hilo moja na kuondoka na ushindi.
Kocha wa Maveterani Mkwawa Bw.Dudu Haruni

Pia kocha wa Iringa Veterani Bw.Haji Omari akielezea namna alivyoibuka na ushindi huo wa bao hilo moja dhidi ya mtani wake Mkwawa Veterani ambapo alisema kitu ambacho kimewafanya wao kushinda katika mchezo huomoja ni  kuelewana kati yake na wachezaji ndani na nje ya uwanja  toka wako mazoezini lakini pia alizungumzia kujiamini ndicho kilichwafanya wao  kuibuka na ushindi huo dhidi ya Maveterani wa Mkwawa.Aidha Captain wa timu hiyo ya Maveterani wa Iringa ambaye ni  Lisa Mwalupindi  kwa upande wake alisema kuwa jambo ambalo lililowafanya kushinda ni kutokana na kuwa na kocha aliye bora pamoja na kuwa na maelewano mazuri na wachezaji wote na kuongeza kuwa wamefurahiswa na ushindi huo wa bao moja kwa bila dhidi ya Maveterani wenzao.


Kocha wa Maveterani Haji Omar

Hata hivyo Bonanza limezikutanisha baadhi ya timu mbalimbali zilizopo kwenye maeneo ya mkoa wa Iringa kama Miomboni Fc.ambao walichuana vikali na ffu.fc na kumaliza mchezo huo kwa kutoshana nguvu ya kutokufungana (bila bila)


Kwa kumaliza  kocha wa Maveterani wa Iringa Bw.Haji Omari alisema kuwa jambo lililowafanya kuvutika katika kuleta bonanza hilo la michezo ni kutokana na mchango wa Mwalimu Jlius Kambarage Nyerere alioutoa wakati wake wa uhai ikiwa ni pamoja na kuhamasisha amani,upendo na kupinga rushwa na kuwasihi wadau mbalimbali,viongozi na wafanyabiashara kudhamini michezo ili vijana waweze kushiriki ambapo utakuwa ni mwanzo mzuri wa kuinua vipaji vyao kwa kujipatia kipato hatimaye na kuwazuia na madawa ya kulevya  hivyo wametumia hii siku katika kumuenzi baba wa taifa katika kuzikutanisha baadhi ya timu mkoa wa Iringa wakiwemo wao wenyewe kama Maveterani wa Iringa.

0 comments: