MFANYABIASHARA wa duka la vipuri vya magari mjini Tarime mkoani Mara, Tumaini Jacob amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akituhumiwa mauaji ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Anadaiwa
kumuua askari huyo wa Kikosi cha Nyandoto, Roja Elias kwa kumpiga
risasi tumboni wakati wakiwa baa moja mjini hapa baada ya kutokea ugomvi
wa kunyang’anyana mwanamke ambaye ni mhudumu wa baa hiyo. Alisomewa
mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime,
Marther Mpaze.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, George Lutonja alidai kuwa Jacob (45) Agosti 17
usiku saa 6 .30 wakati akiwa baa na Hoteli ya NK, kulitokea ugomvi kati
yake na askari huyo.
Alidai
katika ugomvi huo, Tumaini alichomoa bastola yake na kumpiga risasi
Roja tumboni na kutokea mgongoni. Majeruhi huyo alikimbizwa Hospitali ya
Wilaya ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa Hospitali ya
Rufaa Bugando ambapo mauti yalimkuta akipatiwa matibabu katika hospitali
hiyo ya Bugando Mwanza.
Mtuhumiwa huyo Tumaini hakutakiwa kujibu lolote, kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
credit:Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment