Ishu ya imani ni ya mtu binafsi na kila mtu ana uwezo wa kuamini kile anachoona ni sahihi kwa mtazamo wake na mtu anapotokea kumuamini kiongozi wake wa dini kwa asilimia kubwa hutekeleza yale anayofundishwa.
Sasa hii ya leo
inamuhusu mhubiri maarufu wa dini India ambaye ana wafuasi zaidi ya
milioni hamsini duniani Gurmeet Ram Rahim Singh anakabiliwa na mashtaka
ya kusababisha majeruhi kwa tuhuma za kuwashawishi wafuasi wake 400
kukata sehemu zao za siri ili waweze kuwa karibu na Mungu.
Wafuasi
wa Singh walikata sehemu zao za siri kwenye Hospitali ambayo yeye
anaimiliki ambapo kwenye headlines nyingine mhubiri huyu amekuwa
akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi pamoja na
kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia lakini hajawahi kushtakiwa.
Mmoja wa
wafuasi wake, Hans Raj Chauhan aliwaambia Polisi kwamba alikatwa sehemu
zake za siri kwa sababu alidhani asingetakiwa kwenye jamii kama
angekataa kutekeleza utaratibu huo ulioanzishwa Singh.
Singh aliwaambia wafuasi wake kwamba wale ambao wanaotekeleza amri hiyo watakuwa na uwezo wa kumuona Mungu.
0 comments:
Post a Comment