Arsenal huenda ikamkosa beki wake Mathieu Debuchy kwa miezi mitatu kama upasuaji wa bega lake lililoteguka utahitajika.
Beki
huyo wa kulia wa Ufaransa aliumia katika mechi ya ushindi wa 3-0 dhidi
ya Stoke City wiki iliyopita baada ya kusukumwa kwa makusudi na Marko
Arnautovic ambaye amefanikiwa kuepuka adhabu kutoka FA.
Debuchy ataonana na mtaalam ndani yaa masaa 48 yajayo ili kujua kama upasuaji utahitajika au la.
Habari hizi ni pigo kwa Arsenal ambayo safu yake ya ulinzi imekuwa ikiandamwa na majeruhi tangu kuanza kwa msimu huu.
Debuchy
ndiyo kwanza alikuwa anarejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa miezi
mitatu tangu alipoumia kiwiko cha mguu mwezi Disemba.
0 comments:
Post a Comment