Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, August 3, 2015

Mbali na ubabe wake,na kuichukia Marekani_GAIDI,Osama bin laden alikufa akaoza kwa mwanamuziki huyu wa kimarekani_na kusema yupo tayari hata Kuoa



Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden  alizaliwa Machi 10 1957 na kufariki  Mei 2 2011, alikuwa mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaida.


Anatazamwa na watu wengi kama gaidi aliyesababisha vifo vya watu wengi katika mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki (Nairobi na Dar es Salaam) na hasa shambulio la 11 Septemba 2001 huko Marekani.


Ila  wengine wanamwona kama mtetezi wa haki za Waislamu dhidi ya mashambulio ya Marekani akitumia mbinu za jihadi.
Aliuawa na wanajeshi wa Marekani tarehe 2 Mei 2011 nchini Pakistan alipokuwa amefichama.
Mbali na kwamba gaidi huyo alikuwa bandidu,waingereza wakiita badass,na mbali na kuwa alikuwa adui namba moja wa marekani,ila jamaa alikuwa amekufa ameoza kwa mwanamuziki wa kimarekani,hadi kufikia kuapa ikitokea chansi atatangaza ndoa na kumfanya awe kati ya wake zake.




Huyo si mwingine bali ni mwanamuziki aliyekuwa na sauti ya kumtoa nyoka pangoni na mrembo kweli kweli,Witney Huston.



Mwanamama huyu alishafariki na alifariki mwaka mmoja baada ya jeshi la marekani kumuua Osama
AMA kweli mapenzi hayana MACHO

0 comments: